AfyaTrack - Ujauzito na Mtoto

10K+
Downloads
Content rating
Everyone
Screenshot image
Screenshot image
Screenshot image
Screenshot image
Screenshot image
Screenshot image
Screenshot image
Screenshot image

About this app

AfyaTrack App ni application pekee na ya kwanza nchini Tanzania na Afrika Mashariki kukuletea huduma za ufuatiliaji afya mtandaoni kwa lugha ya Kiswahili.

MATUMIZI:
Kwa ujumla application ya AfyaTrack inakuwezesha:

1. Kupata ushauri kwa makala na nyenzo mbalimbali kukusaidia "KUPATA UJAUZITO" wenye afya na kwa wakati.

2. Kufuatilia maendeleo ya "UJAUZITO" wiki hadi wiki tangu kutungwa kwa mimba mpaka kujifungua.

3. Kufuatilia hatua za ukuaji na maendeleo ya afya ya "MTOTO" tangu kuzaliwa mpaka miaka mitano (5).

4. Kujiunga na kuwasiliana na "JAMII" kubwa ya wajawazito na wazazi wengine kwenye mtandao wa AfyaTrack.Com na forums zake kwa ujumla.

KUJIUNGA:
Kujiunga ni rahisi sana. Utahitaji kuwa na E-mail yako, namba yako ya simu na tarehe yako ya kuzaliwa tayari kuweza kujiunga na AfyaTrack app. Baada ya kujiunga na kuingia ndani ya app (Login) utachagua huduma unayotaka kufuatilia halafu ingiza tarehe husika, kisha utapelekwa moja kwa moja kwenye ukurasa wa ufuatiliaji huduma husika.

Unaweza ukabadilisha taarifa za "Account" yako hapo baadae, ikiwemo kubadilisha huduma unayotaka kufuatilia kwa kubonyeza alama ya uso (face icon) iliyopo juu kabisa kulia kwenye app.

HAKI MILIKI:
Taarifa, Makala na Ushauri wowote uliopo kwenye AfyaTrack app na AfyaTrack.Com ni mali ya AfyaTrack. Kunakili, kuchapisha au kushirikisha wengine kwenye tovuti nyingine au mitandao ya kijamii bila kutushirikisha au kuomba idhini kutoka uongozi wa AfyaTrack ni kwenda kinyume na sheria zetu za haki miliki.

ANGALIZO:
Taarifa na maelezo yote yaliyopo kwenye app hii na tovuti ya AfyaTrack.Com yasitumike kubatilisha au kama mbadala wa ushauri na huduma kutoka kwa mtaalamu toka kituo cha afya. AfyaTrack chini ya Afya4All Group inakutahadharisha kuwa haitahusika kwa namna yoyote ile na matokeo ya maamuzi yako utakayochukua kutokana na taarifa hizi zinazotelewa kama taarifa na ushauri kwa jamii yote kwa ujumla.

Taarifa na ushauri huu usitumike kama mbadala wa ushauri utakaopewa na daktari, mkunga au mtoa huduma kutoka kituo rasmi cha afya.

Kama una wasiwasi au tatizo kuhusu ujauzito au mtoto wako tafadhali wasiliana na daktari wako au mtoa huduma wa afya karibu yako.

Timu nzima ya AfyaTrack inakutakia ujauzito mwema, kujifungua salama na malezi mema na afya bora kwako na kwa mtoto wako.

WASILIANA NASI:

Web: http://afyatrack.com
Facebook: http://facebook.com/afyatrak
Twitter: http: @afyatrak
Instagram: @afyatrack

HUDUMA KWA WATEJA:
Tunajitahidi sana kufanya kazi kwa bidii kuboresha huduma za AfyaTrack ili kukuwezesha kupata taarifa sahihi na kwa wakati. Je una ushauri au mawazo ya kutusaidia kuiboresha app hii? Tuandikie barua pepe: feedback@afyatrack.com
Updated on
May 22, 2020

Data safety

Developers can show information here about how their app collects and uses your data. Learn more about data safety
No information available

What's new

**Marekebisho ya Tatizo la Kutohesabu Umri wa Mtoto kwa Usahihi**
Kurekebisha tatizo la baadhi ya watumiaji kushindwa kujiunga
Kuboreshwa kwa muonekano na mfumo wa app kwa ujumla
Kuongezwa kwa huduma ya “KUPATA UJAUZITO”
Kuboreshwa kwa huduma ya “MTOTO”
Kuongezwa kwa Nyenzo (TOOLS)
Uwezo wa kujiunga na JAMII ya wajawazito na wazazi wengine
Jiunge kwa namba ya simu au E-mail
Badili password uliyoisahau kiurahisi