Kithibitishaji cha Google huzalisha nambari za Uthibitishaji wa Hatua Mbili kwenye simu yako.
Kipengele cha Uthibitishaji wa Hatua Mbili kinatoa usalama thabiti kwa Akaunti yako ya Google kwa kuomba uthibitishaji wa hatua ya pili unapoingia katika akaunti. Mbali na nenosiri lako, pia utahitaji nambari ya kuthibitisha itakayozalishwa na programu ya Kithibitishaji cha Google kwenye simu yako.
Pata maelezo zaidi kuhusu Uthibitishaji wa Hatua Mbili: https://g.co/2step
Vipengele:
* Huzalisha nambari za kuthibitisha bila muunganisho wa data
* Kithibitishaji cha Google hufanya kazi katika mitandao ya watoa huduma na akaunti nyingi
* Hutumia Android Wear
* Mandhari meusi yanapatikana
* Uwekji mipangilio kiotomatiki kupitia msimbo wa QR
Ilani ya ruhusa:
Kamera: Inahitajika ili kuongeza akaunti kwa kutumia misimbo ya QR