Sheria na Masharti ya Google Play
Machi 15, 2023 (Angalia toleo lililohifadhiwa kwenye kumbukumbu)
1. Utangulizi
Sheria na Masharti yanayotumika. Asante kwa kutumia Google Play. Google Play ni huduma inayotolewa na Google LLC ("Google", "sisi"), tunapatikana 1600 Amphitheatre Parkway, Mountain View California 94043, Marekani. Matumizi yako ya Google Play na programu (ikijumuisha Programu za Android zinazofunguka papo hapo), huduma za mfumo, michezo, filamu, vitabu, magazeti au maudhui au huduma dijitali (yanayotambulika kama "Maudhui") yanayopatikana kwa njia hii, yanasimamiwa na Sheria na Masharti haya ya Google Play (Sheria na Masharti ya Google Play) na Sheria na Masharti ya Google ("Sheria na Masharti ya Google") (yanayotambulika kwa pamoja kama "Sheria na Masharti"). Google Play ni "huduma" inayofafanuliwa katika Sheria na Masharti ya Google. Ikiwa kuna ukinzani wowote kati ya Sheria na Masharti ya Google Play na Sheria na Masharti ya Google, Sheria na Masharti ya Google Play yatafuatwa.
2. Matumizi yako ya Google Play
Matumizi na idhini ya Kufikia Maudhui. Unaweza kutumia Google Play kuvinjari, kutambua, kuangalia, kutiririsha au kupakua Maudhui katika kifaa cha mkononi, kompyuta, televisheni, saa au kifaa chochote kinachotumika ("Kifaa"). Ili kutumia Google Play, utahitaji Kifaa ambacho kinatimiza mahitaji ya uoanifu na ya mfumo katika Maudhui husika, ufikiaji wa intaneti inayofanya kazi na programu inayoweza kutumika. Upatikanaji wa vipengele na Maudhui utabadilika kulingana na nchi na huenda usipate vipengele au Maudhui yote katika nchi yako. Baadhi ya Maudhui yanaweza kupatikana ili yashirikiwe na wanafamilia. Maudhui yanaweza kutolewa na Google au kuwasilishwa na washirika wengine ambao hawahusiani na Google. Google haiwajibiki au kupendekeza Maudhui yoyote yanayotolewa kupitia Google Play ambayo yanatokana na vyanzo vingine visivyo vya Google.
Vidhibiti vya Umri. Ili uweze kutumia Google Play, ni lazima uwe na akaunti sahihi ya Google ("Akaunti ya Google"), kwa kuzingatia vidhibiti vya umri vifuatavyo. Ikiwa unachukuliwa kuwa mtoto katika nchi yako, ni lazima uwe na ruhusa ya mzazi au mshauri wa kisheria ili utumie Google Play na ukubali Sheria na Masharti. Ni lazima utii vidhibiti vyovyote vya ziada vya umri ambavyo vinaweza kuzingatiwa katika matumizi ya vipengele au Maudhui mahususi kwenye Google Play. Wasimamizi wa familia na wanafamilia ni lazima pia watimize mahitaji haya ya ziada.
Ada ya Washirika Wengine. Utawajibikia ada ya data au ya ufikiaji inayotozwa na washirika wengine (kama vile mtoa huduma ya intaneti au ya simu) kulingana na jinsi unavyotumia na kuangalia Maudhui na Google Play.
Masasisho. Google Play, maktaba husika au Maudhui yanaweza kuhitaji kusasishwa, kwa mfano, kwa ajili ya urekebishaji wa hitilafu, kuboresha utendaji, ukosefu wa programu-jalizi na matoleo mapya (kwa jumla yanaitwa, "Masasisho"). Masasisho kama hayo yanaweza kuhitajika ili uweze kutumia Google Play au upate idhini ya kufikia, kupakua au kutumia Maudhui. Kwa kukubali Sheria na Masharti haya ya kutumia Google Play, unakubali kupokea Masasisho hayo kiotomatiki. Unaweza kudhibiti Masasisho ya Maudhui mengine kupitia Mipangilio katika Google Play. Hata hivyo, ikiwa imebainishwa kuwa Masasisho yatarekebisha athari hatari ya usalama au tatizo kuu la utendakazi linalohusiana na Maudhui, au yatazuia matumizi mabaya, Masasisho yanaweza kukamilika bila kujali mipangilio ya Masasisho katika Google Play au Kifaa chako. Ikiwa programu nyingine itajaribu kusasisha Maudhui ambayo yalipakuliwa awali kutoka Google Play, unaweza kupokea ilani au masasisho kama hayo yanaweza kuzuiliwa kabisa.
Maelezo Yanayokuhusu. Sera ya faragha ya Google inaelezea jinsi tunavyoshughulikia data yako ya binafsi na kulinda faragha yako unapotumia Google Play. Huenda Google ikahitaji utoe maelezo yako ya binafsi, kama vile jina na anwani ya barua pepe, kwa Watoa Huduma kwa sababu za uchakataji wa shughuli au kukupa Maudhui. Watoa Huduma wanakubali maelezo haya kulingana na sera zao za faragha.
Ikiwa wewe ni mshiriki wa kikundi cha familia kwenye Google Play, wanafamilia wanzako katika kikundi wataweza kuona baadhi ya maelezo yanayokuhusu. Ikiwa wewe ni msimamizi wa kikundi cha familia kwenye Google Play, wanafamilia unaoalika kujiunga kwenye kikundi cha familia wataona jina, picha na anwani yako ya barua pepe. Ikiwa utajiunga na kikundi cha familia kuwa mwanafamilia, wanafamilia wengine wataweza kuona jina, picha na anwani yako ya barua pepe. Msimamizi wa familia anaweza kuona umri na pia rekodi ya ununuzi unaofanya ukitumia njia ya kulipa iliyobainishwa ya familia, ikijumuisha maelezo ya Maudhui unayonunua. Ikiwa Maudhui yanapatikana kwa ajili ya kushirikiwa na familia na unayashiriki kwenye kikundi, inamaanisha kuwa wanafamilia wote wataweza kufikia Maudhui hayo na kuona kuwa ni wewe uliyeyanunua.
Ufikiaji Usioruhusiwa wa Akaunti. Ni lazima udumishe usalama wa maelezo ya akaunti yako na hupaswi kuyashiriki na mtu yeyote. Hupaswi kukusanya au kutumia data yoyote ya binafsi ya mtumiaji yeyote wa Google Play au mtumiaji yeyote wa Huduma za Google kupitia Google Play, ikijumuisha majina ya akaunti.
Akaunti Zilizofungwa. Ikiwa Google itafunga idhini ya kufikia akaunti yako kulingana na Sheria na Masharti (kwa mfano ikiwa utakiuka Sheria na Masharti hayo), unaweza kuzuiwa kufikia Google Play, maelezo yako ya akaunti au faili au Maudhui mengine yanayohifadhiwa katika akaunti yako. Tembelea Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi. Ikiwa wewe ni msimamizi wa familia kwenye Google Play na Google ifunge idhini yako ya kufikia akaunti, wanafamilia wako wanaweza kupoteza idhini ya kufikia vipengele vya familia vinavyotumiwa na kikundi cha familia, kama vile njia ya kulipa ya familia, usajili wa familia au Maudhui yanayoshirikiwa na wanafamilia. Ikiwa wewe ni mwanafamilia wa familia kwenye Google Play na Google ifunge akaunti yako, wanafamilia wako watapoteza idhini ya kufikia Maudhui ambayo umeshiriki nao.
Ulinzi dhidi ya programu hasidi. Ili kukulinda dhidi ya programu hasidi, URL na matatizo mengine ya kiusalama kutoka kwa washirika wengine, Google inaweza kupokea maelezo kuhusu muunganisho wa mtandao wa Kifaa chako, URL zinazoweza kuwa hatari, mfumo wa uendeshaji na programu zilizosakinishwa kwenye Kifaa kupitia Google Play au kutoka kwenye vyanzo vingine. Google inaweza kukupa ilani ikiwa itachukuliwa kuwa programu au URL fulani si salama, au Google inaweza kuondoa au kuzuia usakinishaji wa programu hiyo kwenye Kifaa ikiwa inajulikana kuwa hatari kwa Vifaa, data au watumiaji. Unaweza kuchagua kuzima baadhi ya mbinu hizi za ulinzi katika mipangilio kwenye Kifaa chako, hata hivyo Google inaweza kuendelea kupokea maelezo kuhusu programu zilizosakinishwa kupitia Google Play na programu zilizosakishwa kwenye Kifaa kutoka vyanzo vingine zinaweza kuendelea kuchanganuliwa ili kubaini matatizo ya usalama bila kutuma maelezo kwa Google.
Programu za Android Zinazofunguka Papo Hapo. Ukibofya kiungo kwenye Kifaa chako, Google Play inaweza kukagua ikiwa kuna programu inayofunguka papo hapo. Ikiwa ipo, itafungua kiungo ndani ya programu inayofunguka papo hapo. Msimbo wowote unaohitajika kutekeleza sehemu za programu inayofunguka papo hapo unazofikia utapakuliwa kwenye Kifaa chako na kuhifadhiwa hapo kwa muda mfupi. Maelezo ya programu inayofunguka papo hapo yanaweza kupatikana katika Duka la Google Play. Mipangilio na data ya programu za Android Zinazofunguka Papo Hapo husawazishwa kwenye vifaa ulivyotumia kuingia katika akaunti yako ya Google. Unaweza kuchagua kuzima Programu za Android zinazofunguka papo hapo katika mipangilio kwenye Kifaa chako.
Mabadiliko kwenye Sheria na Masharti haya. Ikiwa Sheria na Masharti haya ya Google Play yatabadilika, utapewa ilani ya angalau siku 30 kisha Sheria na Masharti mapya ya Google Play yataanza kutumika baada ya kipindi cha ilani hiyo kuisha. Ukiendelea kutumia Google Play baada ya muda wa ilani kuisha, itaashiria kuwa umekubali Sheria na Masharti mapya ya Google Play. Sheria na Masharti mapya ya Google Play yatatekelezwa katika matumizi yako ya Maudhui yote (ikijumuisha Maudhui ambayo umesakinisha au kununua awali) na Maudhui ambayo utasakinisha au kununua baadaye. Ikiwa hukubali mabadiliko haya, utapewa fursa ya kupakua Maudhui ambayo ulinunua au kusakinisha awali na kusimamisha matumizi yako ya Google Play. Unaweza kuendelea kuangalia nakala ya Maudhui kwenye Vifaa vyako kulingana na toleo la awali la Sheria na Masharti ya Google Play uliyokubali.
3. Ununuzi na Malipo
Maudhui Yasiyolipiwa. Google inaweza kukuruhusu upakue, uangalie au utumie Maudhui yasiyolipiwa kwenye Google Play. Vizuizi vya ziada vinaweza kutumika katika ufikiaji na matumizi ya baadhi ya Maudhui yasiyolipiwa.
Ununuzi wa Maudhui. Unaponunua Maudhui kwenye au ukitumia Google Play utaingia katika mkataba tofauti wa mauzo kulingana na Sheria na Masharti haya (jinsi yanavyotumika) na muuzaji, ambaye anaweza kuwa:
(a) Google Commerce Limited; au
(b) mtoaji wa Maudhui ("Mtoaji"), ikiwemo hali ambapo Google Commerce Limited inatumika kama dalali wa Mtoaji maudhui.
Mkataba tofauti wa mauzo mbali na Sheria na Masharti haya.
Kwa mauzo ambapo Google inatumika kama dalali wa Mtoa Huduma, taarifa, katika Sheria na Masharti ya Google, inayosema kuwa Sheria na Masharti ya Google "haitoi haki zozote za wafaidi wa nje", haitatumika wakati unatumia Google Play.
Mkataba wako wa ununuzi na matumizi ya Maudhui utakamilika baada ya kupokea barua pepe kutoka Google ikithibitisha kuwa ununuzi wako wa Maudhui hayo na utekelezaji wa mkataba huu utaanza pindi ununuzi unapokamilika.
Maagizo ya Mapema. Unapoagiza mapema Maudhui, mkataba wako wa ununuzi na matumizi ya kipengee hicho hukamilika unapopewa Maudhui na utatozwa kwa ununuzi unaofanya wakati huo. Unaweza kughairi agizo la mapema wakati wowote hadi wakati Maudhui hayo yatakapokufikia. Tutahitaji kughairi agizo la mapema ikiwa Maudhui yataondolewa kwenye orodha ya ununuzi kupitia Google Play kabla ya kukufikia na tunahifadhi haki ya kughairi agizo lako bei ikibadilika kabla ya agizo lako kutekelezwa.
Njia ya Kulipa ya Familia. Kama wewe ni msimamizi wa familia wa kikundi cha familia kwenye Google Play, utahitaji kuweka njia sahihi ya kulipa ya wanafamilia wako ili waitumie kununua Maudhui kwenye Google Play na katika programu. Utawajibikia ununuzi wote wa Maudhui unaofanywa na wanafamilia wako kwa kutumia njia ya kulipa ya familia. Ikiwa kikundi cha familia kitafutwa au mwanafamilia ajiondoe kwenye kikundi cha familia, utatozwa kwa ununuzi ambao haujalipiwa uliofanywa na wanafamilia kwa kutumia njia ya kulipa ya familia.
Google Payments. Ili kununua Maudhui kupitia Google Play, ni lazima uwe na akaunti ya Google Payments na ukubali Sheria na Masharti ya Google Payments. Ilani ya Faragha ya Google Payments inatumika wakati unanunua Maudhui ukitumia akaunti ya Google Payments. Unawajibikia malipo yoyote yanayohusiana na ununuzi uliofanywa kupitia Google Play kwenye akaunti yako ya Google Payments.
Njia Nyingine za Kushughulikia Malipo. Mbali na Google Payments, Google inaweza kukuruhusu utumie njia mbalimbali za kushughulikia malipo ili kukuwezesha kununua Maudhui kupitia Google Play. Lazima utii sheria na masharti yoyote yanayohusiana au makubaliano mengine ya kisheria, iwe na Google au watu wengine, yanayosimamia matumizi ya njia husika ya kushughulikia malipo. Google inaweza kuongeza au kuondoa njia za utayarishaji wa malipo kwa hiari yake. Unawajibikia malipo yote yanayohusiana na ununuzi unaofanya kwenye Google Play.
Ustahiki wa Kulipa kupitia Kampuni ya Simu. Ili kubaini ikiwa unaweza kulipia Maudhui unayonunua kwenye Vifaa katika akaunti yako ya mtoa huduma za mtandao, wakati unafungua akaunti ya Google Play kwenye Kifaa, tutatuma vitambulishaji vya Kifaa, kwa mfano Kitambulisho cha mteja na nambari ya ufuatiliaji ya SIM kadi kwa kampuni ya simu unayotumia. Ili kuruhusu hali hii, utahitaji kukubali Sheria na Masharti ya mtoa huduma za mtandao. Mtoa huduma za mtandao anaweza kututumia maelezo yako ya anwani ya kutuma bili. Tutakagua na kutumia maelezo haya kulingana na Sera za Faragha za Google na Ilani ya Faragha ya Google Payments.
Bei. Bei na upatikanaji wa Maudhui yote yanayoonyeshwa kwenye Google Play zinaweza kubadilika wakati wowote kabla ya ununuzi.
Kodi."Kodi" inamaanisha ushuru, ada za forodha, ada zingine zozote (mbali na kodi ya mapato) zinazohusishwa na ununuzi wa Maudhui ikiwemo faini au riba zozote husika. Unawajibikia Kodi zozote na ni lazima ulipie Maudhui bila punguzo lolote la Kodi. Ikiwa muuzaji wa Maudhui au Google analazimika kukusanya au kulipa Kodi, utatozwa Kodi hizo. Ni lazima utii sheria zote au zozote zinazotumika za kodi, ikijumuisha kuripoti na kulipia Kodi zozote zinazotokana na jinsi unavyotumia Google Play au kununua Maudhui kupitia Google Play. Utawajibikia kuripoti na kulipia Kodi zozote zinazotumika.
Mwisho wa Mauzo Yote. Angalia Sera ya Kurejeshewa Fedha ya Google Play ili upate maelezo zaidi kuhusu haki zako za kujiondoa, kughairi au kurejesha bidhaa zozote unazonunua ili urejeshewe pesa. Isipokuwa katika hali ambapo imebainishwa na Sera ya Kurejesha Fedha ya Google Play au sera za Mtoa Huduma za kurejesha pesa, mauzo yote yatakuwa kamilifu, na haturuhusu urejeshaji wa pesa, ubadilishaji au urejeshaji wa bidhaa ulizonunua. Ikiwa ubadilishaji, urejeshaji wa bidhaa au urejeshaji wa pesa unafanyika katika shughuli yoyote, shughuli hiyo inaweza kubatilishwa, na unaweza kukosa kufikia Maudhui ambayo ulipata kupitia shughuli hiyo.
Usajili. Usajili hutozwa kiotomatiki katika kila kipindi cha bili (iwe kila wiki, kila mwezi, kila mwaka au kipindi chochote), na huenda ukatozwa katika muda usio mapema zaidi ya saa 24 kabla ya mwanzo wa kila kipindi cha bili.
(a) Vipindi vya Kujaribu. Ukijisajili katika Maudhui kwa bei fulani, huenda ukapokea idhini ya kufikia manufaa ya usajili bila kutozwa katika kipindi kilichobainishwa, na baada ya kipindi hicho utatozwa hadi utakapoghairi usajili. Ili uzuie kutozwa, ni lazima ughairi kabla ya mwisho wa kipindi cha kujaribu. Baada ya kughairi kipindi cha kujaribu, utapoteza papo hapo idhini ya kufikia Maudhui na manufaa yoyote ya usajili isipobainishwa vinginevyo. Ufikiaji wa vipindi hivyo vya kujaribu unaweza kudhibitiwa kwa idadi fulani ya majaribio kwa kila mtumiaji katika kipindi fulani au vidhibiti vingine.
(b) Kughairi. Unaweza kughairi usajili wakati wowote kabla ya mwisho wa kipindi husika cha bili jinsi ilivyobainishwa katika Kituo cha Usaidizi, na ughairi huo utatumika kwenye kipindi kitakachofuata. Kwa mfano, ukinunua usajili wa kila mwezi, unaweza kughairi usajili wakati wowote wa mwezi huo wa usajili, na usajili utaghairiwa katika mwisho wa kipindi cha sasa cha malipo. Hutarejeshewa pesa katika kipindi husika cha bili isipokuwa jinsi ilivyobainishwa katika Sera ya Google Play ya Urejeshaji Fedha (kwa mfano, katika hali ambapo Maudhui yana hitilafu). (c) Mapunguzo kwa Wateja wa Machapisho. Baadhi ya Watoa Huduma wa majarida wanaweza kuruhusu ununue usajili wa Maudhui ya kipindi fulani kwenye Google Play katika bei iliyopunguzwa ikiwa tayari wewe ni mteja wa chapisho. Ukighairi usajili wako wa chapisho la jarida hilo au muda wa usajili wa chapisho lako uishe na usiusasishe, bei iliyopunguzwa ya usajili wa Maudhui hayo kwenye Google Play itaghariwa kiotomatiki.
(d) Nyongeza ya Bei. Unaponunua usajili, mwanzoni utatozwa bei inayotumika wakati wa makubaliano ya usajili. Ikiwa bei ya usajili itaongezeka baadaye, Google itakuarifu. Ongezeko hili litatekelezwa katika malipo yanayofuata kuanzia wakati unapopokea taarifa, mradi umepewa angalau notisi ya siku 30 kabla ya kutozwa. Ukipewa notisi ya chini ya siku 30, ongezeko la bei halitatekelezwa katika malipo yajayo hadi baada ya wakati wa malipo yafuatayo kufika. Ikiwa hungependa kulipia bei iliyoongezeka ya usajili, unaweza kughairi usajili jinsi ilivyobainishwa katika sehemu ya Kughairi ya Sheria na Masharti haya, na hutatozwa baadaye kutokana na usajili, mradi umetuarifu kabla ya mwisho wa kipindi cha sasa cha bili. Wakati ambapo Mtoa Huduma anaongeza bei ya usajili na idhini inahitajika, Google inaweza kughairi usajili wako usipokubali bei mpya. Ikiwa umeghairi usajili wako na baadaye uamue kujisajili tena, utatozwa bei ya usajili wa wakati huo.
4. Haki na Vikwazo
Leseni ya Kutumia Maudhui. Baada ya kumaliza ununuzi au kulipa ada husika ya Maudhui, utakuwa na haki ya kipekee jinsi inavyoruhusiwa katika Sheria na Masharti haya na sera husika, ili kuhifadhi, kufikia, kuangalia, kutumia na kuonyesha nakala za Maudhui husika kwenye Vifaa vyako au jinsi yalivyoidhinishwa kwa matumizi yako ya binafsi yasiyo ya biashara. Haki zote, mada zote na maslahi yote katika Google Play na Maudhui ambayo hujapewa moja kwa moja kwa mujibu wa Sheria na Masharti yatahifadhiwa. Matumizi yako ya programu na michezo yanaweza kudhibitiwa na sheria na masharti ya ziada ya makubaliano ya mtumiaji wa hatima kati yako na Mtoa Huduma.
Ukiukaji wa Sheria na Masharti ya Leseni. Ukikiuka Sheria na Masharti yoyote, haki zako zilizo chini ya leseni hii zitasimamishwa mara moja, na Google inaweza kusimamisha idhini yako ya kufikia Google Play, Maudhui au Akaunti ya Google bila kukurejeshea pesa.
Vikwazo: Huruhusiwi:
- kuonyesha (chache au yote) Maudhui kama sehemu ya maonyesho au utendaji wa umma hata kama hakuna ada itatozwa isipokuwa (a) hali ambapo matumizi hayo hayatasababisha ukiukaji wa hakimiliki au ukiukaji wa haki yoyote husika au (b) jinsi ilivyobainishwa kwa njia mahususi na kwa njia halisi iliyotolewa.
- kuuza, kukodisha, kusambaza upya, kutangaza, kuwasilisha, kuwasiliana, kubadilisha, kushiriki leseni, kuhamisha, kukabidhi Maudhui yoyote kwa washirika wengine ikijumuisha vipakuliwa vyovyote vya Maudhui unayoweza kupata kupitia Google Play isipokuwa ilingane na ruhusa iliyobainishwa na katika njia halisi tu iliyotolewa.
- kutumia Google Play au Maudhui yoyote kwa pamoja na programu yoyote inayonakili, inayorekodi utiririshaji au programu kama hizo ili kurekodi au kuunda nakala ya Maudhui yoyote unayopata katika muundo wa mtiririko.
- kutumia Maudhui kama njia ya huduma yoyote ya kushiriki, kukodisha au kutumiwa na watu wengi au kwa minajili ya taasisi yoyote, isipokuwa ilingane na ruhusa iliyobainishwa na katika njia halisi tu iliyotolewa.
- kujaribu au kusaidia kuidhinisha au kuhimiza watu wengine kukwepa, kuzima au kuzuia vipengele vyovyote vya usalama ambavyo vinalinda, kuficha au kuzuia ufikiaji wa Maudhui yoyote au Google Play.
- kuondoa alamisho, lebo au ilani zozote za kisheria au za umiliki zinazojumuishwa katika Maudhui yoyote, au kujaribu kubadilisha Maudhui yoyote yanayopatikana kupitia Google Play, ikijumuisha ubadilishaji wowote kwa minajili ya kuficha au kubadilisha ishara zozote za umiliki au chanzo za Maudhui.
Sheria za Washirika Wengine. Bila kujali chochote kinachokinzana na Sheria na Masharti haya, washirika wengine ambao wanatoa idhini ya Maudhui yao katika Google ni wafaidi wa nje chini ya Sheria na Masharti haya kwa kuzingatia kwa njia ya kipekee vifungu mahususi vya Sheria na Masharti haya ambavyo vinahusiana moja kwa moja na Maudhui yao ("Sheria za Mashirika Mengine"), na kwa njia ya kipekee ya kuruhusu washirika wengine kama hao kutekeleza haki zao katika Maudhui kama hayo. Ili kuepuka tashwishi yoyote, hakuna kipengee chochote katika Sheria na Masharti haya kinachowapa wafaidi wa nje haki dhidi ya washirika wowote, kwa kuzingatia sheria yoyote iliyo nje ya Sheria za Washirika Wengine, ambayo inajumuisha sheria au makubaliano yanayojumuishwa na marejeleo, au yanayoweza kurejelewa bila kujumuishwa, katika Sheria na Masharti haya.
Sera za Google Play. Kuchapisha maoni kwenye Google Play kunategemea sera zifuatazo. Ikiwa unataka kuripoti matumizi mabaya au ukiukaji mwingine wa Maudhui, bofya hapa.
Maudhui Yaliyoharibika. Pindi unapotumiwa Maudhui katika akaunti yako, unapaswa kuyakagua haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha kuwa yanafanya kazi jinsi ilivyobainishwa, na utuarifu au umwarifu Mtoa Huduma haraka iwezekanavyo ikiwa utapata hitilafu au uharibifu wowote. Angalia Sera ya Google Play ya Kurejesha Fedha ili upate maelezo zaidi.
Kuondolewa au Kutopatikana kwa Maudhui. Kwa kutegemea Sheria na Masharti, utapata Maudhui ambayo unanunua au kusakinisha kupitia Google Play katika kipindi unachochagua, ikiwa unanunua kwa kipindi cha ukodishaji, na katika hali zingine zozote, mradi Google ina haki ya kukupa Maudhui kama hayo. Katika hali zingine (kwa mfano ikiwa Google itapoteza haki husika, huduma au Maudhui yakatizwe, kuna athari kubwa za usalama, au kuna ukiukaji wa sheria au masharti husika), Google inaweza kuondoa kwenye Kifaa chako au iache kukupa idhini ya kufikia baadhi ya Maudhui ambayo umenunua. Kwa Maudhui yanayouzwa na Google Commerce Limited, huenda ukapewa ilani ya uondoaji au ukomeshaji kama huo, panapowezekana. Ikiwa huwezi kupakua nakala ya Maudhui kabla ya kuondolewa au kukomeshwa, Google inaweza (a) kukupa nakala ya Maudhui ikiwa ipo au (b) kukurejeshea pesa zote au pesa kiasi za Maudhui. Ikiwa Google itakurejeshea pesa, marejesho hayo ya pesa ndiyo yatakuwa suluhu lako pekee.
Akaunti Nyingi. Ikiwa una Akaunti nyingi za Google zinazotumia majina mbalimbali ya watumiaji, katika hali fulani unaweza kuhamisha Maudhui kutoka akaunti moja na kuyapeleka katika akaunti nyingine, mradi wewe ndiwe mmiliki wa kila akaunti na mradi Google imewasha kipengele cha huduma husika kinachoruhusu uhamishaji kama huo.
Vidhibiti vya ufikiaji wa Vifaa. Mara kwa mara, Google inaweza kuweka vidhibiti vya idadi ya Vifaa au programu ambazo unaweza kutumia kufikia Maudhui. Tafadhali tembelea Kanuni za Matumizi ya Filamu na TV kwenye Google Play/Google TV ili upate maelezo zaidi kuhusu vidhibiti hivi kwa Filamu na TV kwenye Google Play/Google TV.
Shughuli Hatari. Hamna Huduma au Maudhui yoyote yanayokusudiwa kutumika katika taasisi za kinyuklia, mifumo ya kulinda maisha, mawasiliano ya dharura, uendeshaji wa ndege, au mifumo ya mawasiliano, mifumo ya kudhibiti safari za ndege au shughuli zozote kama hizo ambapo Huduma au Maudhui yasipofanya kazi yanaweza kusababisha kifo, majeraha ya mwili au madhara hatari ya mazingira.
Filamu na TV kwenye Google Play/Google TV. Ili upate maelezo zaidi na vidhibiti kuhusu ufikiaji na matumizi yako ya Filamu na TV kwenye Google Play/Google TV, angalia Kanuni za Matumizi ya Filamu na TV kwenye Google Play/Google TV.