Chunguza afya yako ndani ya dakika kadhaa kwa app yetu ya afya. Tambua uwezekano wa visababishi vya dalili 24/7 - bila kuhitaji miadi na daktari.
Chochote kinachokusumbua kuanzia matatizo ya tumbo au maumivu makali, ikiwemo maumivu ya kichwa, kikagua dalili chetu cha app ya afya kinaweza kukusaidia kupata majibu bila malipo.
Madaktari wameifundisha app yetu ya afya kwa miaka kadhaa, ili iweze kubaini visababishi vya dalili ndani ya dakika chache.
Madaktari wameifundisha Ada kwa miaka kadhaa, ili uweze kupata utambuzi wa awali wa ugonjwa ndani ya dakika chache.
Uchunguzi wa dalili bila malipo hufanyikaje?
Unajibu maswali rahisi kuhusu afya yako na dalili zilizopo.
Akili Mnemba (AI) ya app yetu ya afya inatathmini majibu yako dhidi ya kamusi yake ya kitiba yenye maelezo ya maelfu ya magonjwa na matatizo ya kiafya.
Unapata ripoti ya tathmini ya afya iliyo maalum kwa ajili yako ambayo inakuambia kinachoweza kuwa kinasababisha dalili zako na nini cha kufanya baada ya hapo.
Nini unachoweza kutarajia kutoka kwenye app yetu?
- Faragha ya taarifa zako (data) na usalama – tunatumia kanuni kali za udhibiti wa data ili kukulinda na kufanya taarifa zako ziwe faragha.
- Majibu sahihi – mfumo wetu wa msingi unaunganisha maarifa ya kitiba na teknolojia erevu.
- Taarifa za kibinafsi za afya – majibu utakayopata kwenye app ni maalum kwa ajili yako kulingana na profaili yako ya kipekee ya afya.
- Ripoti ya tathmini ya afya – mshirikishe daktari wako kwenye taarifa husika ya tathmini yako ya afya kwa kumtumia ripoti yako hiyo katika muundo wa PDF.
- Ufuatiliaji wa dalili – fuatilia dalili zako na kiwango cha ukali wake katika app.
- Makala za masuala ya afya - soma makala maalum zilizoandikwa na madaktari wetu wenye uzoefu.
- Upatikanaji wa huduma 24/7 – unaweza kutumia kikagua dalili cha app yetu ya afya wakati wowote, na mahali popote bila malipo.
- Tathmini za afya katika lugha 7 – changua lugha yako na ibadillishe wakati wowote kupitia mipangilio (settings): Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa, Kiswahili, Kireno, Kihispania, au Kiromania.
Unaweza kuiambia nini app yetu ya afya?
Hakuna maswali yasiyo sahihi. Hizi ni baadhi ya dalili za kawaida unazoweza kuiambia (kwa kuandika) app yetu:
- Homa
- Kupoteza hamu ya kula
- Maumivu ya kichwa
- Maumivu ya tumbo
- Kichefuchefu
- Uchovu
- Kutapika
- Kizunguzungu
- Tumbo kuuma likiguswa
- Kikohozi
Magonjwa yanayoongoza:
- Mafua
- Maambukizi ya homa ya mafua
- Virusi vilivyoathiri mifupa ya pua
- Malaria
- Kisukari
- Maumivu ya kichwa mkazo
- Kipandauso
- Ugonjwa wa Utumbo (IBS)
- Ugonjwa wa wasiwasi kupita kiasi
- Mashambulizi ya hofu
- Sonona
- Klamidia
- Kisonono
- Maambukizi ya hepesi
Makundi ya kawaida:
- Magonjwa ya ngozi, kama vile vipele, chunusi, kuumwa na wadudu
- Afya ya wanawake na ujauzito
- Afya ya watoto
- Afya ya akili
- Magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana
- Hofu ya kupata mimba
- Matatizo ya kukosa usingizi
- Matatizo ya kutomeng’enya chakula tumboni, kama vile kutapika, kuhara
- Maambukizi ya macho
Uboreshaji wa app yetu ya afya ni lengo letu la kudumu, ndiyo maana maoni yako ni muhimu sana kwetu.
TAHADHARI: Ada haiwezi kukupa utambuzi wa matibabu. Wasiliana na huduma ya dharura mara moja katika hali ya dharura. Ada haibadilishi ushauri wa mtaalamu wako wa afya au miadi na daktari wako.
Kama una maoni yeyote, tafadhali wasiliana nasi kupitia hello@ada.com
Ilisasishwa tarehe
8 Okt 2024