Kwa kupitia ECHOcommunity unaweza kugundua maoni, utafiti na mafunzo katika mada anuwai kuhusu ukulima na maendeleo ya kijamii. Rasilimali za ECHO zinalenga kilimo cha kiwango kidogo katika mada na mada ndogo na hutoka kwa wafanyakazi wa ECHO, wanachama wa mtandao, na washirika wa maendeleo kote duniani. Uabiri katika programu unapatikana katika lugha za Kiingereza, Kihispania, Kifaransa, Kiswahili, Kithai, Kirioli cha Haiti, Kikhma, Kibama, Kivietinamu, Kiindonesia, na Kichina.
Programu hii imeundwa kukuruhusu kugundua kwa ufanisi rasilimali zinazofaa na kuzipakua kwenye kifaa chako cha simu. Rasilimali zinazoongezwa kwenye maktaba yako zinaendelea kupatikana wakati hakuna muunganisho wa intaneti na zinaweza kushirikiwa na wengine.
Kipengele cha Rekodi za Mmea cha programu hurekodi matukio ya mzunguko wa maisha ya mazao kutoka kupandwa hadi mavuno. Rekodi za Mmea zinaweza kutumiwa kwa aina yoyote ya upandaji, iwe ni jaribio au upandaji wa uzalishaji, iwe ni wa mwaka au wa kudumu. Watumiaji wanaonunua mbegu kutoka kwa hifadhi za mbegu za ECHO wanaweza kufuatilia na kuripoti maendeleo ya mbegu kwa urahisi wakitumia programu hii.
Programu hii hukuruhusu kurekodi data muhimu kama vile kile unachopanda na wakati wa kupanda, matukio ya hali ya hewa, maingilio kama vile matandazo, ulimajji, kupogoa, na uvunaji. Pamoja na kila ingizo picha na matini yanaweza kuwekwa kwa kumbukumbu za siku zijazo. Data hii inahifadhiwa kwenye wingu, ili uweze kuangalia mbegu ulizojaribu baadaye na jinsi majaribio yalivyokufaa.
Vipengele
- Ufikiaji kwa maelfu ya rasilimali za kuchapisha na video
- Uhifadhi nje ya mtandao na kushirikishwa kwa nyenzo zilizopakuliwa
- Uwezo wa kuuliza maswali wa jamii ya ECHO ulimwenguni
Ilisasishwa tarehe
2 Ago 2024