Kurani ni kitabu kitukufu cha Uislamu ambacho kinatazamwa na Waislamu kama "Neno la Allah (Mwenyezi Mungu)". Kitabu hicho kwao ni tofauti kabisa na maandiko ya dini nyingine kwa maana hicho kinaaminika kwamba kimeandikwa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu, kupitia mtume wake wa mwisho, Muhammad.
Kadiri ya Qurani, Mungu alimuambia Muhammad: "Na namna hivi tumekufunulia Qurani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Makka na walio pembeni mwake"
Kurani imeandikwa na kusomwa kwa lugha ya Kiarabu pekee kwa zaidi ya miaka 1,400.
Lakini, kwa vile leo Waislamu walio wengi ulimwenguni hawajui Kiarabu, maana halisi ya Qur'an hutolewa kwa lugha nyingine, hivyo kupelekea wasomaji kuelewa vyema yale maneno ya Kiarabu kwenye Qur'an yana maana gani. Vitabu hivyo ni kama kamusi kwa ajili ya Qur'an - hawavisomi hivi kama moja ya sehemu ya Quran na Waislamu, ili kuwa badala ya Quran ya Kiarabu.
Waislamu wengi wanaamini kwamba tafsiri ile si ya Qur'an tukufu wala si ya kweli; ni nakala ya Kiarabu tu iliyotolewa kwenye Qur'an ya kweli.
Ilisasishwa tarehe
20 Mac 2022