Appu ya kuhesabu mimba na uzalishaji mifugo humwezesha mtumizi wake kuweka vipimo vya uzaanaji wa mifugo na kuhesabu idadi ya mifugo wenye mimba wanaohitajika na wale wanaopaswa kupewa ndume katika kipindi fulani ili kudhibiti idadi ya mifugo. Mtumizi wa appu hii anapaswa kuanza kwa kuingiza kwenye appu namba ya mifugo wake, kipindi baina ya uzazi mmoja hadi mwingine wa mifugo, kiwango cha upotezaji mimba wa mifugo, kiwango cha uondoaji wa mifugo wasiofaa na kiwango cha vifo miongoni mwa mifugo. Baadaye, mtumizi wa appu hii anafaa kuingiza idadi ya wastani ya ushikaji mimba wa ng’ombe wa kukamuliwa na idadi ya wastani ya ushikaji mimba wa mitama/mori. Ili kupata habari kuhusu data ya nyanjani inayohitajika, unaweza ukarejelea ripoti kwenye programu ya kompyuta iliyo katika shamba
Ilisasishwa tarehe
16 Jul 2025