Drafti Ligi ni drafti ya Kitanzania kwenye simu yako. Cheza mechi za haraka dhidi ya wachezaji kote nchini, panda ligi kila wiki, cheza mechi za ligi na klabu yako na tazama mechi kubwa moja kwa moja.
SHERIA UNAZOZIJUA
Sheria za Kitanzania tangu mwanzo: kete hula mbele tu, wafalme warukao, uhuru wa kuchagua njia ya kula, na kupandishwa cheo humaliza zamu. Programu inaonyesha kila hatua halali na kila ulaji wa lazima, ili uzingatie mchezo.
CHEZA UNAVYOPENDA
• Mechi ya haraka: risasi (1+1), haraka (3+2) au kawaida (10+5), dhidi ya mchezaji wa kiwango chako
• Cheza na kompyuta katika viwango vitano, kutoka Mwanzo hadi Bingwa
• Mpe rafiki changamoto kwa nambari
• Cheza wawili: wachezaji wawili, simu moja
LIGI NA KLABU
• Ligi za kila wiki zenye madaraja, kupanda na kushuka
• Jiunge na klabu, chagueni kikosi na shindeni mechi za ligi pamoja
• Mashindano ya arena na swiss
• Viwango vya kitaifa na vya mikoa
TAZAMA MUBASHARA
Fuatilia bodi za juu zinavyochezwa, toa hisia kwa emoji na rudia michezo iliyokwisha hatua kwa hatua.
UBAO WAKO, MTINDO WAKO
Mbao, kete na viwanja dukani. Pata sarafu kwa kucheza, au nunua almasi.
BURE, HAKUNA KAMARI
Drafti Ligi ni bure kucheza. Hakuna zawadi za pesa wala kamari: washindi hupata alama, vyeo na beji.
Ingia kwa nambari yako ya simu. Inapatikana kwa Kiingereza na Kiswahili.
Drafti ya Kitanzania mtandaoni: mechi za haraka, ligi, klabu na mubashara.
Ilisasishwa tarehe
18 Okt 2026