Endesha biashara yako ya uwakala kidijitali. Pata ripoti za float, shoti, madeni, zamu, makabidhiano, matumizi, faida, kwa usahihi zaidi.
Sifa Zinazotofautisha Wakafy:
📊 Dashibodi ya Mmiliki (Real-time Insights):
Fuatilia mwenendo wa biashara yako (salio, shoti, ziada, faida na matumizi) ukiwa nyumbani au safarini. Pata picha kamili ya biashara yako kwa sekunde.
🤝 Uthibitishaji wa Makabidhiano (Secure Handovers):
Komesha migogoro na "shoti". Mfumo unamtaka anayepewa zamu kuthibitisha kiasi cha float na taslimu kidijitali wakati wa makabidhiano.
🏢 Usimamizi wa Matawi Mengi (Multi-branch Support):
Je, una tawi zaidi ya moja? Unganisha matawi yako yote kwenye akaunti moja na uone utendaji wa kila tawi bila kufika eneo la kazi.
🔐 Usalama wa Hali ya Juu:
Linda taarifa zako za kifedha kwa kutumia alama za vidole (Fingerprint) au utambuzi wa uso (Face ID). Ni wewe tu na watu uliowaruhusu mnaoweza kuingia.
🌍 Lugha Mbili (Bilingual Support):
Chagua lugha unayoipenda; tumia mfumo kwa Kiswahili sanifu au Kiingereza kwa urahisi zaidi.
Mfumo wa usimamizi wa biashara za uwakala wa fedha za simu Tanzania.