KKKT Msharika 365 ni mfumo wa kidijitali ulioundwa kurahisisha huduma za usharika na kuwaunganisha washarika na Kanisa kwa njia rahisi, salama na ya kisasa.
Programu inarahisisha usimamizi na ukusanyaji wa michango, ahadi na shughuli mbalimbali za kifedha zinazohusiana na kampeni na harambee za usharika.
Huduma zinazopatikana
• Michango — Rahisisha ukusanyaji na uwasilishaji wa michango ya washarika.
• Ahadi — Sajili na simamia ahadi za fedha pamoja na ahadi zinazohusiana na minada.
• Harambee na Kampeni — Chagua na kusimamia michango kulingana na harambee au kampeni husika.
• Utambuzi wa Msharika — Tumia namba ya msharika au namba ya simu wakati wa kurekodi huduma husika.
• QR Code — Tumia mfumo wa QR kurahisisha utambuzi na upatikanaji wa taarifa zinazohitajika.
• Huduma hata bila mtandao — Taarifa zinaweza kuhifadhiwa kwa muda pale ambapo mtandao haupatikani na kutumwa kwenye mfumo mtandao unapopatikana tena.
KKKT Msharika 365 inalenga kupunguza matumizi ya mifumo ya karatasi, kurahisisha kazi za kila siku za usharika na kuongeza ufanisi katika utoaji na usimamizi wa huduma.
Teknolojia inayoliweka Kanisa karibu na msharika kila siku.
KKKT Msharika 365 — Usharika wako, siku 365.
Mfumo wa kidijitali wa KKKT kwa kumbukumbu, harambee na huduma za washarika.