Msafiri Plus ni app ya wakala wa mabasi — kata na uza tiketi za safari popote ulipo, hata bila mtandao.
Iwe uko mtaani, kituoni au ndani ya basi, Msafiri Plus inakuwezesha kuhudumia abiria haraka na kwa uhakika. Imejengwa kwa ajili ya mawakala, vituo na kampuni za mabasi Tanzania.
VIPENGELE VIKUU
• Uza popote, hata offline — Endelea kuuza bila mtandao; taarifa husawazishwa zikirudi mtandaoni.
• Chapisha papo hapo — Unganisha printa ya thermal na umpe abiria tiketi kamili kwa sekunde.
• Ratiba za kampuni zote — Safari, nauli, namba za magari na siti zilizobaki mahali pamoja.
• Chagua siti moja kwa moja — Ramani ya siti ya wakati halisi.
• Zuia udanganyifu — QR ya kipekee kwa kila tiketi; tiketi iliyotumika haiwezi kutumika tena.
• Simamia salio na floti yako kwa uwazi.
• Ripoti za kila siku — Mauzo, tiketi, abiria na komisheni kwa muhtasari.
• Ada ya kujiunga: BURE.
Anza kuuza leo. Kwa usaidizi, tupigie 0755 277 133. Imetengenezwa na LOGIX.
Uza tiketi za basi popote, hata offline. Chapisha, skani na pata ripoti.