Vicoba Plus — Kitabu cha Kidijitali cha Kikundi Chako
Vicoba Plus ni zana ya kuweka kumbukumbu za vikundi vya kijamii (VICOBA) mahali pamoja — badala ya madaftari ya karatasi. Programu hii ni kitabu cha kumbukumbu tu: hakuna fedha inayopita ndani ya programu, na haitoi huduma yoyote ya kifedha.
UNACHOWEZA KUFANYA:
• Kusajili kikundi chako na wanachama wake wote
• Kuweka kumbukumbu za michango ya kila mwezi na hisa za wanachama
• Kuandika kumbukumbu za marejesho na madeni ndani ya kikundi
• Kupanga mikutano na kuweka mahudhurio ya wanachama
• Kufuatilia faini za kikundi kulingana na katiba yenu
• Kupata ripoti na muhtasari wa kumbukumbu za kikundi
• Kutumia alama za vidole kuthibitisha utambulisho wa mwanachama kwenye kumbukumbu (kwa ridhaa yake)
INAFANYA KAZI BILA INTANETI
Weka kumbukumbu popote — hata kijijini bila mtandao. Data yako inahifadhiwa kwenye simu na kusawazishwa na seva salama ukipata mtandao.
KWA NANI?
Viongozi wa vikundi vya kijamii, makatibu, wahazini na wanachama wanaotaka kumbukumbu sahihi, salama na za uwazi.
MUHIMU: Vicoba Plus haitoi mikopo, haipokei fedha, haihamishi fedha na haiunganishi watu na watoa huduma za kifedha. Ni kitabu cha kumbukumbu cha kikundi chako.
Sera ya Faragha: http://wesandev.com/privacy_policy
Kitabu cha kidijitali cha kikundi chako - wanachama michango na mgawanyo