Kuhusu kipindi hiki

Hope & Faith ni kipindi cha kuchekesha cha Marekani iliyoonyeshwa kuanzia 26 Septemba 2003 hadi 2 Mei 2006 kwa misimu mitatu kwenye stesheni ya ABC.
Kipindi hiki kilikuwa na waigizaji wakuu: Faith Ford na Kelly Ripa. Hope Shanowski alikuwa na mume na watoto watatu. Faith Fairfield alikuwa muigizaji maarufu na nduguye Hope. Kipindi hiki inatokana na maisha ya mbunifu Joanna Johnson - ambaye alikuwa mhusika katika kipindi maarufu cha The Bold and the Beautiful. Kipindi hiki kilishirikisha wasanii wengine kama Tony Curtis, Dean Cain, Robert Wagner, Regis Philbin, Kathie Lee Gifford, Jenny McCarthy, Jaclyn Smith, Louise McCafferty na Mark Consuelos.
Kipindi hiki kilirekodiwa mjini New York City kwenye Silvercup Studios.