KaPU Chunguza ni programu inayowawezesha wafugaji kuku kutambua dalili za aina tatu za magonjwa ya kuku kwa kupiga picha za kinyesi. Magonjwa yanayoweza kutambuliwa ni Kuhara Damu, Homa ya Matumbo, na ugonjwa wa Kideri. Programu iliandaliwa kwa kutumia modeli ya akili mnemba (AI) na hufanya kazi bila intaneti. Mtumiaji anapakia kwenye programu picha ya kinyesi cha kuku au anapiga picha ya kinyesi hicho. Kisha, programu hutoa majibu ya aina ya ugonjwa au kinyesi kuwa bila ugonjwa (afya).