Ukiwa na Cryptomator, ufunguo wa data yako uko mikononi mwako. Cryptomator husimba data yako kwa njia fiche haraka na kwa urahisi. Baada ya hapo unazipakia zikiwa zimehifadhiwa kwenye huduma yako uipendayo ya wingu.
RAHISI KUTUMIACryptomator ni zana rahisi ya kujilinda kidijitali. Inakuwezesha kulinda data yako ya wingu peke yako na kwa kujitegemea.
• Unda hifadhi ya data na ugawanye nenosiri
• Hakuna akaunti ya ziada au usanidi unaohitajika
• Fungua hifadhi ya data kwa kutumia alama ya kidole chako
INAOANACryptomator inaoana na hifadhi za wingu zinazotumika sana na inapatikana kwa mifumo yote mikubwa ya uendeshaji.
• Inaoana na huduma za hifadhi ya wingu zinazotegemea Dropbox, Google Drive, OneDrive, S3- na WebDAV.
• Unda vihifadhi katika hifadhi ya ndani ya Android (k.m., inafanya kazi na programu za kusawazisha za wahusika wengine)
• Fikia vihifadhi vyako kwenye vifaa vyako vyote vya mkononi na kompyuta.
SALAMAHuna haja ya kuamini Cryptomator bila kujua, kwa sababu
ni programu huria. Kwako kama mtumiaji, hii ina maana kwamba kila mtu anaweza kuona msimbo.
• Maudhui ya faili na usimbaji fiche wa jina la faili kwa kutumia AES na urefu wa ufunguo wa biti 256.
• Nenosiri la vihifadhi limelindwa na scrypt kwa ajili ya upinzani ulioimarishwa wa nguvu kali.
• Vihifadhi hufungwa kiotomatiki baada ya kutuma programu chinichini.
• Utekelezaji wa Crypto umerekodiwa hadharani.
USHINDI WA TUZOCryptomator ilipokea Tuzo ya Ubunifu ya CeBIT 2016 kwa Usalama na Faragha Zinazotumika. Tunajivunia kutoa usalama na faragha kwa mamia ya maelfu ya watumiaji wa Cryptomator.
JUMUIYA YA CRYPTOMATORJiunge na
Jumuiya ya Cryptomator na ushiriki katika mazungumzo na watumiaji wengine wa Cryptomator.
• Tufuate kwenye Mastodon
@cryptomator@mastodon.online• Tupende kwenye Facebook
/Cryptomator