Hebu fikiria kuwa unaweza kuhifadhi Wikipedia nzima kwenye simu yako, na kuivinjari wakati wowote, mahali popote, hata wakati hakuna muunganisho. Nje ya mtandao kabisa! Kwa bure!
Kiwix ni kivinjari kinachopakua, kuhifadhi na kusoma nakala za tovuti zako za elimu uzipendazo - Wikipedia, mazungumzo ya TED, Stack Exchange, na maelfu zaidi katika lugha nyingi.
Kumbuka: Kiwix inapatikana pia kwenye kompyuta za kawaida (Windows, Mac, Linux) na pia kwenye maeneo-pepe ya Raspberry Pi - maelezo zaidi katika
kiwix.org . Kiwix ni shirika lisilo la faida na haionyeshi matangazo wala kukusanya data yoyote. Michango kutoka kwa watumiaji wenye furaha pekee ndiyo hutufanya tuendelee :-)