Utoaji Mimba Salama (UMS)

3.2
Maoni 843
elfu 100+
Vipakuliwa
Daraja la maudhui
Kila mtu
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini

Kuhusu programu hii

Zana hii inatoa taarifa pana na rafiki kwa mtumiaji juu ya utoaji mimba salama. Inatoa taarifa za afya kwa njia inayoeleweka, isiyohukumu na yenye vielelezo vingi.
Zana hii ina kikokotoo cha wiki za mimba kusaidia wale wanaohitaji kusitisha ujauzito kujua njia mbalimbali zilizopo, na taarifa zinazoeleweka zenye vielelezo juu ya matarajio kutokana na utoaji mimba salama kwa njia ya vidonge, ufyonzaji (MVA), na D&E, na jinsi ya kushughulikia changamoto pale zinapojitokeza.

Zana ya Utoaji Mimba Salama imesanifiwa kulinda faragha ya mtumiaji, kutumiwa na mtu akiwa pekee yake au kuwashirikisha marafiki, wafanyakazi wa afya na wanaharakati wa afya ya wanawake. Pale inapopakuliwa, zana hii hufanya kazi bila kuhitaji data au intaneti. Kwa kuwa inatoa taarifa za kuaminika, kueleweka na za kivitendo, zana hii inaweza kusaidia kuzuia madhara yanayosababishwa na utoaji mimba usio salama na vikwazo vinavyokwamisha upatikanaji wa afya ya uzazi.

Menyu kuu ya zana hii ipo juu, kona ya kulia ya safu ya pinki. Tumia menyu kuzuru sehemu na taarifa zote muhimu za zana, zikiwemo:

1. “Kadiria mimba ina wiki ngapi,” kwa kutumia kikokotoo cha wiki za mimba. Ingiza tarehe ya kuanza hedhi yako ya mwisho kubaini ujauzito wako una wiki ngapi. Zana itachambua njia gani ya utoaji mimba salama inakufaa zaidi, njia zingine zinazoweza kukufaa, na zipi hazikufai.

2. “Taarifa muhimu” hutoa taarifa ambazo unahitaji kujua juu ya utoaji mimba kwa njia ya vidonge, zikiwa na viunganishi ili kujifunza zaidi kupitia zana hii.

3. “Taarifa za nchi yako” huelezea hali halisi ya kisheria na kutoa viunganishi kwa mashirika ya ndani na ya kimataifa ambayo yanaweza kusaidia.

4. “Njia za Utoaji Mimba Salama” na “Kulinganisha Njia” huelezea na kulinganisha njia za utoaji mimba kwa vidonge, ufyonzaji na D&E.

5. “Utoaji Mimba kwa Vidonge” huelezea dozi sahihi na jinsi ya kutumia misoprosto (pamoja au bila mifepristoni) kwa ajili ya utoaji mimba zenye wiki tofauti kwa dawa. Pia inaelezea dozi sahihi za dawa ya kichefuchefu, na za kupunguza maumivu ambazo zinaweza kuhitajika.

6. “Dalili za hatari” huelezea ufanye nini kama kuna homa, maumivu makali au utokaji damu, au dalili zingine zenye kutia hofu, pamoja na viashiria vingine kwamba msaada wa kitabibu au dharura unahitajika haraka.

7. “Anza Uzazi wa Mpango” huelezea njia tofauti za kukuepusha usipate mimba.

8. Sehemu ya “FAQs” imebeba mambo mengi na inatoa majibu kwa zaidi ya maswali 30 juu ya taratibu na wasiwasi kuhusu utoaji mimba.

9. “Nyenzo zaidi'' inajumuisha viunganishi kwa nyenzo za video, mtandao na machapisho juu ya afya ya uzazi, ukatili wa kijinsia na zaidi.

Kwa kuchagua nyota juu ya ukurasa, watumiaji wanaweza kuhifadhi(bookmark) ukurasa huo. Utapata ukurasa huo na kurasa zingine zilizohifadhiwa kwa kuchagua ikoni ya nyota kwenye safu ya chini ya rangi ya chungwa.

Alama ya sauti inayosikika kwenye safu ya chini ya rangi ya chungwa hukuruhusu kuanza kusoma kwa sauti.

Safu ya kutafuta ya rangi ya chungwa juu huruhusu watumiaji kutafuta taarifa mahsusi haraka au kutumia mshale kurudi nyuma kwenye ukurasa uliopita.

Zana hii inapatikana katika lugha ya Afaan Oromoo, Amharic, Kiingereza, Kireno, Kifaransa, Ki Igbo, Kinyarwanda, Kiswahili, Luganda na Ki Yoruba. Kubadili lugha, chagua ikoni ya giya kwenye kona ya juu kulia na kuchagua lugha inayotaka.

Bofya ikoni ya giya kujifunza zaidi juu ya Hesperian Health Guides, kujifunza juu ya sera ya faragha, kupata msaada katika kutumia zana hii, na kuwapatia wengine zana kwa njia ya barua pepe, andiko au mitandao ya kijamii.

Katika kipindi hiki ambapo upatikanaji wa haki na huduma za afya ya uzazi unazidi kukwazwa,hii ndiyo zana ambayo ulikuwa unaisubiri!
Ilisasishwa tarehe
23 Apr 2024

Usalama wa data

Usalama huanza kwa kuelewa jinsi wasanidi programu wanavyokusanya na kushiriki data yako. Faragha ya data na mbinu za usalama zinaweza kutofautiana kulingana na matumizi yako, eneo ulilopo na umri wako. Msanidi programu ametoa maelezo haya na anaweza kuyasasisha kadiri muda unavyopita.
Hakuna data inayoshirikiwa na wengine
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi wasanidi programu wanavyobainisha kushiriki data
Hakuna data iliyokusanywa
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi wasanidi programu wanavyobainisha ukusanyaji wa data

Ukadiriaji na maoni

3.2
Maoni 839

Mapya

Sasisho ndogo za yaliyomo