Msaragambo

4.6
Maoni elfu 15.5
1M+
Vipakuliwa
Daraja la maudhui
Miaka 12 kwenda juu
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini

Kuhusu programu hii

Jibu maswali rahisi na ya kufurahisha yanayokuwezesha kupata manufaa makubwa! Piga hatua katika viwango tofauti, pata beji na ushiriki mafanikio yako kadiri unavyochangia! Michango yako isiyo ya lazima hufanya bidhaa za Google kuwa bora katika eneo unaloishi. Ifundishe programu ya Mratibu wa Google kuelewa vizuri maana, kuboresha lugha yako katika Google Tafsiri na kuisadia huduma ya Picha kwenye Google kutambua vitu. Hizi ni baadhi ya aina tofauti za michango inayokua kwa kasi ambayo unaweza kuchangia ili kuboresha bidhaa za Google katika maeneo ya karibu na duniani kote.



Jaribu baadhi ya majukumu haya ili ujiunge na jumuiya ya wachangiaji ya Google:



Uthibitishaji wa Mwandiko: Tujulishe iwapo mwandiko unalingana na maandishi unayoyaona.

Usomaji wa Mwandiko: Tujulishe iwapo unaweza kutambua kilicho kwenye mwandiko.

Ulinganishaji wa Mwandiko: Linganisha mitindo miwili ya mwandiko na uchague unaoupendelea.

Uthibitishaji wa Sehemu: Thibitisha kuwa fokasi ipo juu ya kitu unapopiga picha.

Ulinganishaji wa Vyakula: Linganisha sifa za picha mbili za vyakula.

Mchango wa Sauti: Rekodi sauti yako ili uboreshe teknolojia ya matamshi.

Ukweli kuhusu Chakula: Tupatie maelezo ikiwa mlo una sifa mahususi.

Lebo za Vyakula: Tuambie picha ina chakula gani.

Ulinganifu wa Kisemantiki: Kagua ikiwa sentensi mbili zina maana moja.

Uelewa kuhusu Chati: Kagua ikiwa chati zinaeleweka na zinaaminika.

Kuandika kwa Kutelezesha Kidole: Telezesha vidole vyako kwenye kibodi ili uandike maandishi unayoyaona.

Uthibitishaji wa Sauti: Sikiliza klipu fupi ya sauti na ubaini ikiwa matamshi ya lugha yako yametamkwa kwa ufasaha.

Maelezo ya Picha: Rekodi sauti yako ikielezea picha zinazowasilishwa kwako ili kuboresha teknolojia ya matamshi.

Uthibitishaji wa Lebo za Picha: Tuambie ikiwa picha zimewekewa lebo kwa usahihi.

Kupiga Picha: Piga na ushiriki picha za matukio yanayotokea mahali ulipo.

Tafsiri: Tafsiri maneno na vifungu vya maneno katika lugha mbalimbali.

Uthibitishaji wa Tafsiri: Chagua vifungu vya maneno ambavyo vimetafsiriwa kwa usahihi.

Utambuzi wa Mwandiko: Angalia mwandiko na uandike maandishi unayoyaona.

Kutathmini Hisia: Bainisha ikiwa sentensi iliyo katika lugha yako kama ina hisia chanya, hasi au isiyoegemea upande wowote.

Kamera Mahiri (Toleo la Android Lollipop 5.0 au toleo jipya zaidi linahitajika): Elekeza kamera kwenye kitu unacholenga ili uone kama inaweza kukitambua.



Kila mara unapowasilisha majibu, unafanya bidhaa za Google ziwafae watu wote kwa miaka mingi ijayo. Pia, utazawadiwa manufaa kutokana na usaidizi wako, kama vile kuwasiliana na wachangiaji wengine kwenye mikutano ya mahali ulipo, kupokea mialiko mahususi ya kushiriki Hangouts za mtandaoni na WanaGoogle pamoja na wachangiaji wengine na kuangaziwa kwenye mifumo ya kijamii ya Msaragambo. Ikiwa uko katika kituo cha basi, kwenye foleni au ndani ya treni, chukua muda kidogo kuboresha bidhaa za Google kwa ajili ya jumuiya yako.
Ilisasishwa tarehe
13 Feb 2024

Usalama wa data

Usalama huanza kwa kuelewa jinsi wasanidi programu wanavyokusanya na kushiriki data yako. Faragha ya data na mbinu za usalama zinaweza kutofautiana kulingana na matumizi yako, eneo ulilopo na umri wako. Msanidi programu ametoa maelezo haya na anaweza kuyasasisha kadiri muda unavyopita.
Programu hii huenda ikashiriki aina hii ya data na watu wengine
Taarifa binafsi
Programu hii huenda ikakusanya aina hizi za data
Mahali, Taarifa binafsi na nyingine5
Data inasimbwa kwa njia fiche inapotumwa
Unaweza kuomba data hiyo ifutwe

Ukadiriaji na maoni

4.6
Maoni elfu 15

Mapya

Marekebisho ya vifaa vya Android 14 yanayohusu kupakua miundo ya Kamera ya kutumia kwenye Kamera Mahiri na katika majukumu ya Kunasa Picha