Programu rasmi ya Studio ya YouTube ndiyo njia bora zaidi ya kukusaidia kuwafahamu na kuwasiliana na watu katika jumuiya yako kwa kutumia kifaa ulichozoea. Tumia programu hii:
- Kupata muhtasari wa haraka kuhusu utendaji wa maudhui na kituo chako kwenye Dashibodi mpya ya Kituo.
- Kufahamu utendaji wa kituo chako na aina nyingine za maudhui kupitia Takwimu za kina. Unaweza pia kuona data ya utendaji wa aina mbalimbali za maudhui katika kichupo cha Takwimu.
- Kukuza uhusiano wa kina na hadhira yako kupitia uwezo wa kupanga na kuchuja maoni ili kupata mazungumzo muhimu zaidi katika jumuiya yako.
- Kufanya mabadiliko kwenye mwonekano na muundo wa kituo chako na kudhibiti aina mahususi za maudhui kwa kusasisha maelezo ya video fupi, mitiririko mubashara na video mahususi.
- Kuanzisha biashara kwenye YouTube kwa kutuma ombi la kujiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube ili uweze kuchuma mapato.
Ilisasishwa tarehe
30 Mei 2024
Vihariri na Vicheza Video