Kikuza Sauti

3.8
Maoni elfu 74.2
100M+
Vipakuliwa
Daraja la maudhui
PEGI 3
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini

Kuhusu programu hii

Kikuza Sauti hufanya sauti za mazingira na mazungumzo ya kila siku kupatikana kwa urahisi zaidi na watu wenye tatizo la kusikia, kwa kutumia tu simu yako ya Android na vipokea sauti vya kichwani. Tumia Kikuza Sauti ili uchuje, uongeze na ukuze sauti karibu nawe na kwenye kifaa chako.

Inapatikana kwa vifaa vinavyotumia Android 8.1 na zaidi. Ili uanze kutumia Kikuza Sauti, unganisha vipokea sauti vyako vya kichwani kisha uende kwenye Mipangilio > Ufikivu > Kikuza Sauti au Mipangilio > Ufikivu > Programu zilizopakuliwa.

Vipengele
• Punguza kelele zisizotakiwa ili uyatambue vizuri matamshi.
• Makinika na sauti ya mzungumzaji katika mazingira ya kelele kwa kutumia kipengele cha hali ya mazungumzo. (Inapatikana kwa Pixel 3 na matoleo mapya zaidi.)
• Sikiliza mazungumzo, TV au mihadhara. Kwa vyanzo vya sauti ambavyo viko mbali, vipokea sauti vya kichwani vya Bluetooth vinapendekezwa. (Vipokea sauti vya kichwani vya Bluetooth vinaweza kupokea sauti kwa kuchelewa.)
• Wekea mapendeleo hali yako ya usikilizaji wa mazungumzo yanayokuzunguka au maudhui yanayocheza kwenye kifaa chako. Unaweza kupunguza kelele au kuboresha sauti za masafa ya chini, masafa ya juu au sauti tulivu. Wekea mapendeleo yako masikio yote mawili au tenganisha kwa kila sikio.
• Washa na uzime huduma ya Kikuza Sauti kwa kutumia kitufe cha zana za ufikivu, ishara au Mipangilio ya Haraka. Pata maelezo zaidi kuhusu kitufe cha zana za ufikivu, ishara na Mipangilio ya Haraka: https://support.google.com/accessibility/android/answer/7650693
• Fungua Kikuza Sauti kwa urahisi zaidi kwa kukiongeza kwenye orodha yako ya programu. Katika mipangilio ya Kikuza Sauti, washa “Onyesha aikoni kwenye orodha ya programu”.

Mahitaji
• Inapatikana katika toleo la Android 8.1 au toleo jipya zaidi.
• Oanisha kifaa chako cha Android na vipokea sauti vya kichwani.
• Kwa sasa kipengele cha hali ya mazungumzo kinapatikana kwenye Pixel 3 na toleo jipya zaidi.

Tutumie maoni yako kuhusu huduma ya Kikuza Sauti kwa kutuma barua pepe kwenye: sound-amplifier-help@google.com. Kwa usaidizi wa jinsi ya kutumia Kikuza Sauti, wasiliana nasi kupitia https://g.co/disabilitysupport.

Arifa ya Ruhusa
Maikrofoni: Ufikiaji wa maikrofoni utaruhusu huduma ya Kikuza Sauti ichakate sauti kwa ajili ya ukuzaji na uchujaji. Hakuna data inayokusanywa au kuhifadhiwa.
Huduma ya Ufikivu: Kwa kuwa programu hii ni huduma ya ufikivu, inaweza kuangalia shughuli zako, kuleta maudhui ya dirisha na kuona maandishi unayoandika.
Ilisasishwa tarehe
5 Feb 2024

Usalama wa data

Usalama huanza kwa kuelewa jinsi wasanidi programu wanavyokusanya na kushiriki data yako. Faragha ya data na mbinu za usalama zinaweza kutofautiana kulingana na matumizi yako, eneo ulilopo na umri wako. Msanidi programu ametoa maelezo haya na anaweza kuyasasisha kadiri muda unavyopita.
Hakuna data inayoshirikiwa na wengine
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi wasanidi programu wanavyobainisha kushiriki data
Programu hii huenda ikakusanya aina hizi za data
Taarifa binafsi, Sauti na nyingine3
Data inasimbwa kwa njia fiche inapotumwa
Data haiwezi kufutwa
Ukaguzi huru wa usalama

Ukadiriaji na maoni

3.8
Maoni elfu 73.2
Gibole Gweso
30 Oktoba 2023
Iko vizuri
Mtu mmoja alinufaika kutokana na maoni haya
Je, maoni haya yamekufaa?
បងម៉ៅ ឃាវ៉ា
30 Januari 2022
"Carro"
Watu 3 walinufaika kutokana na maoni haya
Je, maoni haya yamekufaa?