Google Kids Space

3.7
Maoni elfu 3.27
10M+
Vipakuliwa
Zimeidhinishwa na Walimu
Daraja la maudhui
Kila mtu
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini

Kuhusu programu hii

Google Kids Space ni kipengele kinachotumika kwenye kishikwambi kikiwa na skrini ya kwanza maalum na maktaba yenye maudhui bora kwa ajili ya watoto wenye umri wa chini ya miaka 9. Watoto wanaweza kubadilisha wapendavyo hali zao za utumiaji kwa kutumia ishara maalum na kupokea mapendekezo ya maudhui kulingana na mambo yanayowavutia, wakati wazazi wanaweza kuweka mipaka ya matumizi kwa kutumia kipengele cha vidhibiti vya wazazi.

Google Kids Space huhitaji Akaunti ya Google ya mtoto wako na kifaa oanifu cha Android.


Michezo na programu zilizoidhinishwa na walimu
Google Kids Space inajumuisha programu na michezo kutoka Google Play ambayo imeidhinishwa na walimu na wataalamu wa elimu pamoja na maudhui ya watoto. Programu Zilizoidhinishwa na Walimu zina maudhui yanayoambatana na umri, zimebuniwa kwa umakini na zinafurahisha au kuhamasisha.

Kwa wazazi wanaohitaji uhuru wa kufikia maudhui zaidi ya yale yanayopendekezwa na Google Kids Space, wanaweza kuongeza maudhui zaidi kutoka duka la Google Play kupitia menyu ya wazazi.

Vitabu vilivyochaguliwa na wataalamu wa vitabu vya watoto
Orodha kutoka Vitabu vya Google Play, iliyobuniwa na wataalamu imeratibiwa kikamilifu ili kuhamasisha utaratibu wa kujisomea vitabu. Kupitia vitabu na wahusika wanaovutia, kuna vitabu vya kawaida na hadithi mpya zinazohusu mada kuanzia malori hadi bale. Watoto wanaweza kupata mambo mapya yanayowavutia au kutembelea tena baadhi ya hadithi wanazozipenda tena na tena.

Video zinazopendekezwa zilizo na maudhui muhimu
Watoto wanaweza kuhamasika kubuni, kugundua na kufanyia mazoezi ujuzi wao kwa kutumia video kutoka YouTube Kids ambazo zinachochea ubunifu na kufanya kwa vitendo. Watapata video kuhusu kila kitu kuanzia shughuli rahisi za uchoraji hadi miradi ya sayansi inayokuza ubunifu. Iwe wanataka kujifunza, kuimba au kucheka, watoto wanaweza kugundua video kuhusu mada na wahusika wanaowapenda.

Imebuniwa kwa kuzingatia udadisi wa watoto
Iwe ni miradi ya wanyama au sanaa, watoto huwa wataalamu wadogo kwenye mambo wanayopenda. Google Kids Space imebuniwa kuwasaidia watoto kugundua mambo ya sasa yanayowavutia na kujifunza zaidi, wakitumia mbinu mpya na shirikishi. Watoto wanaweza pia kuweka mapendeleo ya hali zao za utumiaji kwa kubuni wahusika wao wenyewe, watakaoonekana kwenye skrini wanapoingia katika akaunti.

Weka mipaka kwa kutumia vidhibiti vya wazazi
Kwa kutumia vidhibiti vya wazazi kwenye programu ya Family Link kutoka Google, unaweza kusimamia matumizi ya mtoto wako kwa kudhibiti maudhui kutoka Google Play, kuweka ukomo wa muda wa kutumia kifaa na zaidi, yote haya kwa kutumia kifaa chako.

Maelezo muhimu
Google Kids Space hubadilisha skrini ya kwanza ya kishikwambi cha mtoto wako kwa hali inayomsaidia kupanga maudhui anayoyafahamu na kuyapenda katika vichupo vya programu na michezo, video na vitabu. Google Kids Space inaweza kuzimwa wakati wowote kwenye menyu ya mzazi.

Kipengele cha Google Kids Space huhitaji Akaunti ya Google ya mtoto wako. Vidhibiti vya wazazi vinahitaji kifaa kinachoweza kutumia programu ya Family Link kwenye Android, Chromebook au iOS. Upatikanaji wa vipengele unaweza kutofautiana kulingana na eneo. Google Kids Space inapatikana kwenye vishikwambi mahususi vya Android. Programu ya Mratibu wa Google haipatikani katika Google Kids Space.

Huenda vitabu na maudhui ya video yasipatikane katika maeneo yote. Maudhui ya video yanategemea upatikanaji wa programu ya YouTube Kids. Maudhui ya vitabu yanahitaji programu ya Vitabu vya Google Play. Upatikanaji wa programu, vitabu na maudhui ya video unaweza kubadilika bila ilani.
Ilisasishwa tarehe
1 Jul 2024

Usalama wa data

Usalama huanza kwa kuelewa jinsi wasanidi programu wanavyokusanya na kushiriki data yako. Faragha ya data na mbinu za usalama zinaweza kutofautiana kulingana na matumizi yako, eneo ulilopo na umri wako. Msanidi programu ametoa maelezo haya na anaweza kuyasasisha kadiri muda unavyopita.
Hakuna data inayoshirikiwa na wengine
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi wasanidi programu wanavyobainisha kushiriki data
Programu hii huenda ikakusanya aina hizi za data
Taarifa binafsi, Maelezo ya fedha na nyingine3
Data inasimbwa kwa njia fiche inapotumwa
Unaweza kuomba data hiyo ifutwe
Kujitolea kufuata Sera ya Familia ya Google Play
Ukaguzi huru wa usalama

Ukadiriaji na maoni

3.5
Maoni 422

Mapya

Hitilafu kadhaa zimerekebishwa na uthabiti kuboreshwa