Weka mipangilio na udhibiti Pixel Buds zako kwenye kifaa chako cha Android 6.0+ ukitumia Programu ya Google Pixel Buds. Unaweza kuangalia kwa urahisi viwango vya betri ya kipochi na vifaa vyako vya sauti vya masikioni na kudhibiti vipengele kama vile Sauti Inayojirekebisha, utambuzi wa ndani ya sikio, tafuta kifaa, Mratibu wa Google na arifa za kutamkwa.
Hivi ni baadhi ya vitu unavyoweza kufanya ukitumia Programu ya Google Pixel Buds:
• Kuangalia viwango vya betri
• Kujifunza jinsi ya kutumia vidhibiti vya kugusa
• Kuwasha/kuzima Sauti Inayojirekebisha
• Kuwasha/kuzima utambuzi wa ndani ya sikio
•Piga vifaa vyako vya sauti vya masikioni ili ikusaidie kuvipata
• Kudhibiti Mratibu na arifa za kutamkwa
• Kupata vidokezo na usaidizi
Kufungua Programu ya Pixel Buds:
• Kwenye Pixel, unganisha vifaa vyako vya sauti vya masikioni > Mipangilio ya Bluetooth > gusa ⚙️kando ya Pixel Buds.
• Kwenye simu nyingine za Android, tafuta aikoni ya Programu ya Pixel Buds kwenye Skrini yako ya kwanza.
Kumbuka: Programu hii ni ya Google Pixel Buds (Toleo la pili)
Ilisasishwa tarehe
6 Mac 2024