Kufikia kwa Swichi

4.1
Maoni elfu 13.2
100M+
Vipakuliwa
Daraja la maudhui
Kila mtu
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini

Kuhusu programu hii

Dhibiti simu au kompyuta kibao yako ukitumia swichi au kamera ya mbele. Unaweza kutumia swichi kuchagua vipengee, kusogeza, kuandika na zaidi.

Kipengele cha Kufikia Kupitia Swichi hukusaidia utumie kifaa chako cha Android ukitumia swichi moja au zaidi badala ya skrini ya kugusa. Kipengele cha Kufikia Kupitia Swichi kinaweza kukusaidia ikiwa huwezi kutumia kifaa chako moja kwa moja.

Ili uanze kutumia:
1. Fungua programu ya Mipangilio ya kifaa chako.
2. Gusa Zana za Ufikivu > Kufikia Kupitia Swichi.

Weka mipangilio ya swichi

Kipengele cha Kufikia Kupitia Swichi huchanganua vipengee kwenye skrini yako na kuangazia kila kipengee hadi utakapochagua. Unaweza kuchagua kutoka kwenye aina kadhaa za swichi:

Swichi halisi
• Swichi za USB au Bluetooth, kama vile vitufe au kibodi
• Swichi zilizo kwenye kifaa, kama vile vitufe vya sauti

Swichi za Kamera
• Achama mdomo, tabasamu au inua nyusi zako
• Tazama kushoto, kulia au juu

Changanua kifaa chako

Baada ya kuweka mipangilio ya swichi, unaweza kuchanganua na kutumia vipengee vilivyo kwenye skrini.

• Uchanganuzi kwa mstari: Sogeza kati ya vipengee, kimoja baada ya kingine.
• Uchanganuzi wa safu mlalo-safu wima: Changanua safu mlalo moja baada ya nyingine. Baada ya safu mlalo kuchaguliwa, kagua vipengee vilivyo kwenye orodha hiyo.
• Uchanganuzi wa sehemu mahususi: Tumia mistari inayosogea ili uchague eneo mahususi la mlalo na wima, kisha bonyeza "Chagua".
• Uteuzi wa kikundi: Weka swichi kwenye vipengee tofauti vya rangi. Vipengee vyote kwenye skrini vitawekewa rangi. Bonyeza swichi inayolingana na rangi karibu na kipengee unachotaka. Punguza ukubwa wa kikundi hadi utakapofikia chaguo lako.

Tumia menyu

Kipengele kinapoteuliwa, utaona menyu zilizo na matumizi yaliyopo, kama vile kuteua, kunakili, kubandika na zaidi.
Pia kutakuwa na menyu katika sehemu ya juu ya skrini ili kukusaidia usogee kwenye kifaa chako. Kwa mfano, unaweza kufungua arifa, kwenda kwenye skrini ya kwanza, kubadilisha sauti na zaidi.

Sogeza kwa kutumia Swichi za Kamera

Unaweza kutumia Swichi za Kamera kusogea kwenye simu yako ukitumia ishara za uso. Kuvinjari au kuchagua programu kwenye simu yako kwa kutumia kamera ya mbele ya simu yako.
Pia, unaweza kuweka mapendeleo ya ung'avu na muda wa kila ishara kulingana na mahitaji yako.

Njia za mkato za kurekodi

Unaweza kurekodi ishara za kugusa ambazo zinaweza kuwekwa kwenye swichi au kuanzishwa kwenye menyu. Ishara za kugusa zinaweza kujumuisha kubana, kukuza, kusogeza, kutelezesha kidole, kugusa mara mbili na zaidi. Kisha unaweza kuanzisha vitendo changamano na vya mara kwa mara kwa kutumia swichi moja, kwa mfano, kurekodi ishara inayotelezesha kushoto mara mbili ili kugeuza kurasa mbili za kitabu pepe.

Ilani ya Ruhusa
• Huduma ya Ufikivu: Kwa sababu programu hii ni huduma ya ufikivu, inaweza kujifunza vitendo vyako, kuleta maudhui ya kidirisha na kujifunza maandishi unayoandika.
Ilisasishwa tarehe
21 Ago 2023

Usalama wa data

Usalama huanza kwa kuelewa jinsi wasanidi programu wanavyokusanya na kushiriki data yako. Faragha ya data na mbinu za usalama zinaweza kutofautiana kulingana na matumizi yako, eneo ulilopo na umri wako. Msanidi programu ametoa maelezo haya na anaweza kuyasasisha kadiri muda unavyopita.
Hakuna data inayoshirikiwa na wengine
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi wasanidi programu wanavyobainisha kushiriki data
Programu hii huenda ikakusanya aina hizi za data
Taarifa binafsi, Ujumbe na nyingine4
Data inasimbwa kwa njia fiche inapotumwa
Data haiwezi kufutwa
Ukaguzi huru wa usalama

Ukadiriaji na maoni

4.1
Maoni elfu 12.9

Mapya

Sasisho hili linajumuisha kurekebishwa kwa hitilafu.