Tunakuletea Gallery, programu mahiri, nyepesi na inayofanya kazi haraka. Inahifadhi picha na video na imebuniwa na Google ili ikusaidie:
✨ Kutafuta picha haraka kwa kuzipanga kiotomatiki
😎 Kuboresha picha zako kwa kutumia zana za kuhariri picha kama vile uboreshaji wa kiotomatiki
🏝️ Kutumia data kidogo - hufanya kazi nje ya mtandao na ni programu ndogo isiyotumia nafasi kubwa
KUPANGA KIOTOMATIKI
Kila usiku, Gallery itapanga kiotomatiki picha zako katika kikundi kulingana na: Watu, Selfi, Maumbile, Wanyama, Hati, Video na Filamu.
Gallery hukusaidia kupanga maudhui yako, ili utumie muda mchache kutafuta picha ya rafiki au mwanafamilia na muda mwingi zaidi kushiriki nao matukio.*
UBORESHAJI WA KIOTOMATIKI
Gallery ina zana za kuhariri picha zilizo rahisi kutumia, kama vile uboreshaji wa kiotomatiki utakaofanya picha zipendeze zaidi kwa kubofya mara moja.
UWEZO WA KUTUMIA FOLDA NA KADI ZA SD
Tumia folda kupanga picha katika njia yoyote ile unayopenda. Yote haya bado ukiwa na uwezo wa kutazama, kunakili na kuhamishia kwenye na kutoka Kadi za SD kwa urahisi.
UTEKELEZAJI
Gallery huwa katika faili ndogo, hali inayomaanisha kuwa picha zako zitakuwa na nafasi kubwa zaidi ya hifadhi. Haya yote hufanyika huku ikitumia hifadhi ndogo kwenye kifaa chako - kwa hivyo haitapunguza kasi ya simu yako.
HUFANYA KAZI NJE YA MTANDAO
Gallery imeimarishwa ili ifanye kazi nje ya mtandao, inaweza kudhibiti na kuhifadhi picha na video zako zote bila kutumia data yako yote.
*kipengele cha kupanga picha katika makundi kulingana na nyuso za waliomo hakipatikani katika nchi zote kwa sasa
Ilisasishwa tarehe
17 Jan 2024