Kwa vifaa na vitu vyako
• Angalia simu, kishikwambi, vipokea sauti vya kichwani na vifuasi vyako vingine kwenye ramani–hata iwapo havipo mtandaoni.
• Cheza sauti ili upate kifaa chako kilichopotea iwapo kipo karibu.
• Ikiwa umepoteza kifaa, unaweza kufuta data yote iliyomo au kukilinda kutoka mbali. Unaweza pia kuweka ujumbe maalum utakaoonekana kwenye skrini iliyofungwa endapo mtu atapata kifaa chako.
• Tafuta vifaa na vitu vyako kwenye Simu na vifaa vinavyotumika vyenye Wear OS.
• Data yote ya mahali katika mtandao wa Kitafutaji husimbwa kwa njia fiche. Data hii ya mahali haionekani hata kwa Google.
Kuruhusu ufikiaji wa data ya mahali
• Ruhusu ufikiaji wa data ya mahali ulipo katika muda halisi ili upange kukutana na rafiki au uthibitishe iwapo mwanafamilia alifika nyumbani salama.
Ilisasishwa tarehe
15 Des 2025