Zana za Ufikivu za Android ni mkusanyiko wa programu za ufikivu zinazokusaidia utumie kifaa chako cha Android bila kukitazama au kwa kutumia kifaa cha swichi.
Zana za Ufikivu za Android ni pamoja na:
• Menyu ya Ufikivu: Tumia menyu hii kubwa iliyo kwenye skrini ili kufunga simu yako, kudhibiti kiwango cha sauti na mwangaza, kupiga picha za skrini na zaidi.
• Chagua ili Izungumze: Chagua vipengee kwenye skrini yako na usikie vikisomwa kwa sauti.
• Kisoma skrini cha TalkBack: Pata maelezo yanayotamkwa, dhibiti kifaa chako ukitumia ishara na uandike ukitumia kibodi ya nukta nundu iliyo kwenye skrini.
Ili uanze kutumia:
1. Fungua programu ya Mipangilio kwenye kifaa chako.
2. Chagua Ufikivu.
3. Chagua Menyu ya Ufikivu, kipengele cha Chagua ili Izungumze au TalkBack.
Arifa ya Ruhusa
• Simu: Zana za Ufikivu za Android zinaangalia hali ya simu ili kuyafanya matangazo yaendane na hali ya simu unayopiga.
• Huduma ya Ufikivu: Kwa sababu programu hii ni huduma ya ufikivu, inaweza kuchunguza vitendo unavyotekeleza, kuleta maudhui yaliyo kwenye dirisha na kuona maandishi unayoandika.
• Arifa: Unaporuhusu ruhusa hii, TalkBack inaweza kukuarifu kuhusu masasisho.
Ilisasishwa tarehe
30 Sep 2025