Huduma hii hukuwezesha kutumia kompyuta kibao au simu yako ya Android kudhibiti Android TV yako. Badilisha kwa urahisi kati ya hali ya d-pad na padi ya kugusa ili usogeze maudhui na ucheze michezo kwenye kifaa chako cha Android TV. Gusa maikrofoni ili uanze kutafuta kwa kutamka, au utumie kibodi kuandika kwenye Android TV.
Ili uanze kutumia, unganisha kompyuta kibao au simu yako ya Android kwenye mtandao unaotumiwa na kifaa chako cha Android TV, au utafute Android TV yako kupitia bluetooth.
Hutumika kwenye vifaa vyote vya Android TV.
Ilisasishwa tarehe
7 Jul 2025