Ikiwa na Fitbit iliyojumuishwa, saa yako ni zana thabiti ya kukusaidia ufikie malengo yako ya afya na siha. Panga siku yako na kiwango cha shughuli kulingana na kipengele cha Muhtasari wa Asubuhi, ambako unaweza kuona maarifa muhimu, alama yako ya utayari, vipimo vya afya na malengo ya kila siku. Pia, pata vidokezo vitakavyokusaidia kufuata mienendo bora ya afya, kama vile vikumbusho unapokaa bila kusogea kwa muda mrefu.
Zifuatazo ni baadhi ya programu nyingine zinazofanya shughuli za kujitunza ziwe rahisi zaidi, iwe ni utaratibu wako wa asubuhi na ulaji wa vyakula vyenye lishe au kupumzika.